SERENGETI BREWERIES LTD
RE: TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
SBL
YAMZWADIA MKAZI WA MBAGALA LIMO BAJAJI YA 5
Kampuni ya
bia ya Serengeti Breweries leo imetoa zawadi ya Limo Bajaji kwa Bw. Mfaume
Hassan Lwembe (43) ambaye ni dereva taxi na mkazi wa Mbagala katika kampeni yake
inayoendelea ya “Tutoke na Serengeti”. Hii imetangazwa leo katika droo inayofanyika
kila wiki makao makuu ya SBL yaliyopo Chang’ombe jijini Dar es Salaam chini ya
usimamizi wa PWC na bodi ya michezo ya
bahati nasibu Tanzania.
“Ninafuraha sana kusikia habari hizi, Asante
sana Serengeti” alisema Bw. Mfaume mara baada ya kupewa taarifa za kuibuka
mshindi wa Limo Bajaj kwenye promosheni ya Tutoke na Serengeti. Aliendelea
kusema kwamba...“Hatimaye sasa nimepata kitu ambacho kitanisaidia kuinua hali
ya maisha yangu”.
Alipoulizwa
njinsi alivyoshiriki kwenye promosheni hiyo, Mfaume alieleza kwamba … “Baada ya
kazi, huwa napendelea kupumzika sehemu na rafiki zangu huku tukipata vinywaji.
Tangu promosheni hii ianze, nimekuwa nikinunua Serengeti Premium Lager na mara
kwa mara nimekuwa nikituma namba zilizo chini ya kizibo kwenda 15317 kwa njia
ya ujumbe mfupi. Ninamshukuru Mungu siku
ya leo juhudi zangu zimezaa matunda leo”.
Mfaume
aliipongeza SBL kwa kuwa kampuni ya kwanza kuanzisha promosheni ya aina hii
hapa nchini, na kuuthibitishia umma kuwa promosheni hii ni halali kabisa na
hakuna uchakachuaji katika kumpata mshindi.
Akiongea
na vyombo vya habari, Meneja chapa bia ya Serengeti Premium Lager Bwana. Eli
Huruma Ngowi alisema “kutokana na uhitaji na muitikio mzuri kutoka kwa wateja wetu
kwenye kampeni hii”, SBL imeongeza mwezi mmoja wa promosheni ili kutoa fursa
kwa wateja wengi zaidi kujishindia zawadi mbalimbali zilizoorodheshwa hapo
awali….Kwa mantiki hiyo basi kampeni hii itafika kikomo mwisho wa mwezi Februari
tofauti na ilivyotarajiwa mwanzo kuwa ingeisha mwezi Januari.
Eli
Huruma aliendelea kusema kwamba “Hadi sasa zaidi ya shilingi milioni 700 tayari
zimeshatumika katika kuwazawadia washindi mbalimbali ambapo kati yao watu (5) wameshinda
Limo Bajaj na (2) wameshinda ziara ya kutembelea hifadhi ya taifa ya Serengeti
national park huku wateja wengi zaidi wamejishindia fedha taslim Tsh 100,000 zinazotelewa
kila wiki baada ya droo.
“SBL
pamoja na BPESA wanajivunia kwamba promosheni hii imebadilisha maisha ya watu
wengi kwa kiasi kikubwa ” alimalizia Eli Huruma.
Kwa
upande mwingine, taarifa kutoka ofisi za BPESA, wataalam wa teknolojia ambao
katika promosheni hii wanahusika na usambazaji wa fedha kwa njia ya simu kwa
washindi kutoka pande mbalimbali hapa nchini,
wamethibitisha kuwa watamkabidhi Bw. Mfaume Bajaj yake wiki ijayo.
Ili
kushiriki kwenye promosheni hii, mteja anatakiwa awe na umri wa zaidi ya miaka
18, anunue Serengeti Premium Lager na kuangalia chini ya kizibo ambapo atakuta
namba ambazo anatakiwa kuzituma kwenda katika mamba 15317. Kadiri mteja
anavyoshiriki, ndivyo anavyojiweka katika nafasi ya kushinda.
-MWISHO-
KWA MAELEZO
ZAIDI TEMBELEA:-
Kurasa za Serengeti premium Lager
Face book/Twitter na YouTube kwa video.
KUHUSU
SERENGETI BREWERIES LIMITED
Serengeti Breweries Limited
inajihusisha na utengenezaji, uandaaji, uuzaji na usambazaji wa vinywaji vya
kimea na shayiri na uwele hapa Tanzania.
Ikiwa na makao makuu yake hapa Dar es
Salaam, bidhaa za Serengeti ni pamoja na:- Serengeti Premium Lager, Serengeti
Platinum, Tusker Lager, Tusker Lite, Kibo Gold, Uhuru Peak Lager, Pilsner
Lager, Senator, The Kick na Guinness®..
No comments:
Post a Comment