Gazeti la Daily mail limemuumbua mshambuliaji kutoka nchini Italia pamoja na klabu ya Liverpool, Mario Balotelli kwa kuanika picha zake mtandaoni, saa chache baada ya mchezo wa ligi kuu ya soka nchini England ambao ulishuhudia The Reds wakiibuka na ushindi wa mabao mawili kwa sifuri dhidi ya Aston Villa mwishoni mwa juma lililopita.
Balotelli, hakuwa sehemu ya kikosi cha Liverpool kwa siku hiyo kwa kisingizio cha kuwa majeruhi, lakini baadae alionekana katika mgahawa wa San Carlo huko mjini Manchester sambamba na mashabiki wake.
Pamoja na kuwa na uhuru wa kutembelea sehemu starehe licha ya kuwa majeruhi bado Balotelli alionekana ni mwenye furaha na hakuonyesha kama ni mgonjwa hali ambayo imezua maswali mengi miongoni mwa wadau wa soka walioziona picha hizo kwa kuhisi huenda hakuwa mkweli.
Katika mchezo dhidi ya Aston Villa, Liverpool walijipatia mabao yao ya ushindi kupitia kwa Fabio Borini pamoja na Rickie Lambert.
No comments:
Post a Comment