Kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za serikali- PAC imeiagiza mamlaka ya bandari nchini kurejesha fedha zote za usafiri zilizolipwa kwa wafanyakazi wake tangu mwaka 2011, kabla ya kuidhinishwa.
Hayo yameelezwa jana na mwenyekiti wa kamati ya PAC Zitto Kabwe ambaye amebainisha kuwa kumekuwepo na viashiria vya matumizi mabaya ya fedha yanayofanywa na baadhi ya wafanyakazi wasio waaminifu bila kufuata miongozo sahihi.
Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa kamati hiyo Deo Filikunjombe amesema katika mikutano mbalimbali waliyofanya wamebaini tatizo kubwa la ukosefu wa nyaraka za uthibitisho wa matumizi ya fedha zinazotumika.
Naye mjumbe wa kamati hiyo Ismail Aden Rage, ameitaka mamlaka ya bandari pamoja na mamlaka nyingine kutoridhika na adhabu ya kuwasimamisha kazi wafanyakazi wanaobainika kuhusika na matumizi mabaya ya fedha badala yake wawafilisi au kuwafungulia mashtaka
No comments:
Post a Comment