KOCHA BORA WA MWAKA WA FIFA KWA SOKA LA WANAUME
Tuzo hii kwa mara ya kwanza ilitolewa mwaka 2010 ambapo Jose Mourinho alikuwa wa kwanza kushinda akiwa Inter Milan. 2011 Pep Guardiola alishinda akifuatiwa na Vicente Del Bosque mwaka 2012 na anayeshikilia tuzo hiyo ni Jupp Heynckes.
…………………………………………………………
MKUTANO NA WANAHABARI: KIPI KINAMFANYA MTU KUWA KOCHA BORA?
CARLO ANCELOTTI
“Kitu muhimu ni kufanya kazi kwa bidii,, uwezo wa kufanya kazi kwa pamoja. Ni jitihada kubwa. Lazima mtu awe mvumilivu”.
JOACHIM LOW
“Nadhani kocha anahitaji kuwa mwana saikolojia. Kuiweka pamoja timu. Naamini kuwa haya ndio majukumu makubwa ya kocha, kuona ni watu wa aina gani unao”
DIEGO SIMEONE
“Ningependa kuzungumzia kuhusu ushindani wa ndani kuwa ndio kitu muhimu. Kuwa katika kikosi kinachoanza, ndipo unawaona wachezajinwako. Kuwa katika makombe, ligi na ligi ya mabingwa. Njia bora ni kuwa tayari kuwa na ushindani wa ndani ya timu”.
……………………………………………………………..
SIMEONE KARIBU ANACHUKUA NAFASI YAKE
Diego Simeone ambaye anawania tuzo ya kocha bora wa mwaka katika mpira wa wanaume anakaribia kujiunga na wapinzani wake wengine Carlo Ancelotti na Joachim Low kwenye mkutano na waandishi wa habari. Tayari alishapiga picha yake.

CRISTIANO RONALDO YUPO KWENYE NDEGE
Nyota anayetetea tuzo yake, Christiano Ronaldo yupo njiani kuja Zurich na muda si mrefu atawasili hapa.
Wachezaji wa FC BAYERN Manuel Neuer pamoja na Arjen Robben wapo kwenye ndege ya kukodi kuja hapa Zurich kwenye tuzo,Neuer anawania tuzo ya mwanasoka bora pamoja na kina Ronaldo na Messi.
Wachezaji wa FC BAYERN Manuel Neuer pamoja na Arjen Robben wapo kwenye ndege ya kukodi kuja hapa Zurich kwenye tuzo,Neuer anawania tuzo ya mwanasoka bora pamoja na kina Ronaldo na Messi.
Kocha wa zamani wa Fc Bayern Munich na Borussia Dortmund Otmar Hizzified anampa nafasi Mjerumani mwenzake Neuer kubeba tuzo ya Ballon D’Or.
Andres Iniesta na Lionel wapo kwenye ndege wanakuja kwenye tuzo,
No comments:
Post a Comment