Huyu ni Baraka kijana mrefu kitanzania |
Inasemekana ni kijana mrefu kuliko wote Tanzania. Kijana huyu (katikati pichani) ambaye anadhaniwa ni mrefu kuliko vijana wote Tanzania anaishi maeneo ya Gongolamboto, Banana jijini Dar es salaam. Kijana huyu huwa haonekani sana mitaani, lakini aliingia mjini siku hiyo na kuleta kizaa zaa kikubwa pale alipoibuka mitaa ya Aggrey, Kariakoo. Alikuwa kivutio kwa kila aliyemuona, alifunga mtaa watu wakimshangaa na kumgombania kupiga nae picha. Kila aliyetaka kupiga nae picha alitoa Shilingi elfu moja Tsh. 1000.
Picha hiyo amepigwa ndani ya Kinyozi (Salon) aliyoingia kupunguza nywele zake na umati wa watu walikuwa nje ya kinyozi huyo kumsubiri atoke. Mpaka sasa hajajulikana jina lake kamili na anafanya nini. Inasemekana kuna watu wanamfuatilia kumsaidia umaarufu.
Hapa Hasheem Thabit alipokutana na Baraka |
JULIUS CHARLES |
UKIMUANGALIA kwa mara ya kwanza mchezaji wa Tanzania anayecheza
timu ya kikapu ya Oklahoma City Sounders inayoshiriki Ligi ya Kikapu
Marekani (NBA), Hasheem Thabit unaweza kujiridhisha kwamba ni mrefu
kuliko Watanzania wote uliowahi kuwaona. Ana futi 7.3.
Lakini mjini Bagamoyo katika Mkoa wa Pwani kwenye
shule ya Lord Barden yupo mchezaji anayemzidi Hasheem kwa urefu akiwa na
futi 7.5. Si mwingine namzungumzia Julius Charles (18) ni maarufu zaidi maeneo ya
Bagamoyo, na umaarufu huo umetokana na kimo chake huku wengi wakimuita
mpinzani wa Hasheem Thabit kutokana na urefu alionao ambao umepitiliza
na ukikutana naye lazima utishike au ubaki ukimshangaa.
No comments:
Post a Comment