Mwanadada anayefanya vizuri kwenye muziki na uigizaji wa filamu Bongo, Tiko Hassan.
Leo mwandishi wetu Gladness Mallya amemnasa mwanadada anayefanya vizuri kwenye muziki na uigizaji wa filamu Bongo, Tiko Hassan. Unataka kujua ameulizwa maswali gani na akajibu vipi? Fuatilia hapa chini.
Ijumaa: Wasanii wengi mna tabia ya kuwa na wapenzi zaidi ya mmoja, yaani yupo wa kukupa fedha, wa mapenzi na wa kujirusha tu sehemu mbalimbali za starehe, vipi kwako likoje hili?
Tiko: Ukweli mimi huwa nikiwa na mwanaume mmoja natulia naye huyohuyo, tukiachana ndiyo nakuwa na mwingine, hiyo tabia ya kuwa na wanaume wengi sina na siipendi kabisa.
Tiko: Tabia hii inakera sana na ni ushamba. Mimi sijawahi kumchukua mwanaume wa mtu maana najiamini kama mwanamke, wanaotuharibia sifa ni hao wengine maana lisemwalo lipo.
Ijumaa: Kuna tetesi kwamba wasanii wengi mnafanya mapenzi kinyume na maumbile ili wapenzi wenu wasiwaache, wewe umeshawahi?
Tiko: Sijawahi kufanya wala sifikirii maana hata vitabu vya dini vinakataza, huwa natumia uanamke wangu kumridhisha mpenzi wangu lakini siyo kufanya uchafu huo.
Ijumaa: Je, unakwepaje vishawishi vya wanaume wakware mtaani ambao wakiona wasichana warembo kama wewe hutumia nguvu zote kuwanasa?
Tiko: Huwa nakaza moyo na ninafikiria mbele zaidi maana najua wapo watu nyuma yangu wanaoniangalia na kunitegemea hivyo inanipa nguvu ya kuvishinda vishawishi.
Ijumaa: Siku hizi matumizi ya dawa za Kichina za kuongeza makalio na matiti yamezidi, je ulishawahi kutumia?
Tiko: Hivi unanionaje? Cheki nilivyo, kufungashia huku ni kwa asili na hata matiti yangu pia hayana uhusiano na dawa za Kichina. Waliozaliwa hawana shepu ndiyo wanaohangaika.
Ijumaa: Hivi mpaka sasa umeshatoka na wanaume wangapi?
Tiko: Ukweli sikumbuki wanaume niliotoka nao maana idadi yao mh!
Ijumaa: Ni changamoto gani unazokutana nazo kwenye kazi yako ya muziki na filamu?
Tiko: Changamoto zipo nyingi tu, wapo wanaotukatisha tamaa lakini kwa kuwa tumedhamiria kwenye fani, naamini tutashinda.
Ijumaa: Kuna wanaosema wewe huwezi kuimba ila unafuata mkumbo, hilo unalizungumziaje?
Tiko: Ndiyo changamoto ninazozizungumzia hizo, kama siwezi kuimba mbona kazi zangu zinakubalika mtaani? Hayo ni maneno ya watu wasiopenda maendeleo yangu.
Ijumaa: Sasa hivi umeelekeza nguvu zako kwenye muziki, vipi filamu umeacha?
Tiko: Filamu sijaacha na siwezi kuacha ila kwa sasa macho yangu yapo zaidi kwenye muziki.
Ijumaa: Kuna hizi rushwa za ngono kwa wasanii wanaoingia kwenye fani ya muziki na filamu hasa kwa wasichana, wewe hujakumbana na kutakwa ili ‘ushaini’?
Tiko: Kikubwa ni kuwa na msimamo, hayo mambo yapo lakini inategemea unajiwekaje, ukijirahisi wanakupitia kweli
No comments:
Post a Comment