Mrembo
ambaye alikuwa mpenzi wa Star wa klabu ya Liverpool Fanny Neguisha
amefichua chanzo cha kuachana na mchezaji huyo baada ya kimya cha muda
mrefu .
Baloteli
na Fanny walionekana kuwa pamoja kwa muda mrefu kabla ya kuachana baada
ya muda huku kukiwa hakuna sababu iliyowahi kutajwa na yoyote kati ya
wapenzi hao wa zamani ya kuachana kwao .
Balotelli
alifikia hatua ya kumchumbia binti huyo raia wa Ubelgiji mwenye asili
ya Ethiopia akimvisha pete ya thamani ya paundi elfu 25,000 wakati
wakiwa nchini Brazil .
Mwanadada
huyo amefichua kuwa chanzo cha wawili hao kuachana na kitendo cha Mario
Baloteli kumlazimisha aachane na fani yake ya uanamitindo pamoja na
muziki .
Fanny
amefichua kuwa Balotelli alikuwa hapendezewi na picha za mitindo ambazo
alikuwa akipiga , kimsingi hakuwa anakubaliana na kazi yake hali
iliyofanya arudishe pete yake ya uchumba na kusitisha mipango yao ya
kuoana.
Baloteli hakutaka Mpenzi wake Fanny Neguisha ajihusishe na kazi ya urembo na mitindo pamoja na muziki .
Fanny alisema hayo kwenye mahojiano ya tele
visheni
ambapo alisema kuwa Baloteli alimlazimisha aachane na mitindo , ambapo
mrembo huyo alisisitiza kuwa anaipenda kazi yake na ana haki ya kuwa na
maisha ya kazi kama ilivyo kwake (Balotelli) jambo ambalo Mario
hakukubaliana nalo
No comments:
Post a Comment