Rais Jakaya Kikwete ana mchango mkubwa kwenye maisha ya Rehela Chalamila
aka Ray C. Kwa kutambua hilo, Ray C anatarajia kumpa zawadi maalum kwa
moyo wake aliouonesha kuokoa maisha ya muimbaji huyo aliyewahi kuwa
mtumiaji wa dawa za kulevya.
Ray C amekiambia kipindi cha The Mboni Show cha TBC1 kuwa hana zawadi
kubwa zaidi ya kumpatia JK zaidi ya kuandaa show kubwa na kumkaribisha
kuwa mgeni rasmi.
“Kwa ukweli sina uwezo wa ukweli wa kumpa chochote kile,” alisema Ray C.
“Lakini nachojua kitu alichoniambia ni kwamba ‘nitafurahi sana ukirudi
kwenye muziki na utaendelea na shughuli yako’ nikamwambia ‘baba
nitafanya hivyo,” aliongeza.
“Kwahiyo nimeweza kurekodi album nzima na ninategemea nifanye show kubwa
sana ambayo nitamwita yeye awe mgeni rasmi na nina uhakika siku
atakayoniona kwenye stage atajua kweli nimerudi, kweli aliokoa kipaji.
Maana yake ameokoa kipaji, watanzania walishanizoeana na nadhani
ningeondoka kwa style ile nadhani ningewaumiza sana mashabiki wangu.
Nashukuru nimerudi ni ni mzima wa afya.”
No comments:
Post a Comment