Katika hali isiyotarajiwa, mchumba wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul
‘Diamond’, Wema Sepetu na aliyewahi kuwa mchumba wa msanii huyo, Penniel
Mungilwa ‘Penny’ walikutana studio na kila mmoja akamkwepa mwenzake.
Tukio hilo lilitokea juzikati maeneo ya Posta, jijini Dar katika Studio
za Amaya ambayo ni saluni inayotumika kurekodia vipindi mbalimbali vya
Mkasi vinavyorushwa kupitia Runinga ya EATV.
Kwa mujibu wa chanzo
makini, mwigizaji Aunt Ezekiel alialikwa na mtangazaji wa kipindi hicho,
Salama Jabir kwenda kufanya mahojiano, akaambatana na shosti wake Wema
ndipo ghafla wakakutana na Penny ambaye naye alialikwa kwa wakati wake.
Chanzo
kilizidi kumwaga data kuwa, baada ya Aunt na Wema kufika studio hapo,
Salama aliwakaribisha na wakaanza kurekodi kipindi hicho, lakini
walipokuwa wakiendelea na mahojiano, Penny naye aliwasili bila kujua
kama Wema alikuwepo.
“Penny alipofika alizama ndani na kukutana na
Salama ambaye alimwambia kuwa kuna watu wanatoka ndani muda si mrefu
hivyo wakati bado wanaongea, Wema na Aunt walitoka studio ambapo Penny
alikimbilia kwenye gari lake kukwepa kuonana na Wema ambaye pia
alionekana kutotaka kuonana na Penny,” kilisema chanzo na kuongeza:
“Kwa kuwa Wema naye alimuona kwa mbali Penny, alimtaka Aunt waingie kwenye gari fastafasta na kuondoka eneo hilo.”
Mapaparazi wetu baada ya kuunyaka mchongo huo, walimtafuta Penny ili
kumsikia anazungumziaje ishu hiyo. Alipopatikana, alijibu hivi:
“Mimi
sikumkimbia Wema na itambulike kuwa wakati naenda pale sikujua kama
Wema alikuwepo hivyo nilifika na kusubiria muda wangu wa mahojiano
nikiwa ndani ya gari, sikuwa na haja ya kujua Wema yupo ama la.”
Jitihada za kumpata Wema hazikuzaa matunda lakini alipotafutwa Aunt Ezekiel, alitiririka:
“Nilimuona
Penny kweli pale studio ingawa mwanzo nilitahamaki maana sikujua kama
naye alikuwa akisubiria tutoke aingie kwenye kipindi ila Salama
alinishtua sana baada ya kusema kabla hatujatoka ndani tusubiri aandae
uwanja wa ngumi, alitania.”
Wema na Penny wanadaiwa kuwa picha
haziendi baada ya Wema kumtuhumu Penny ambaye alikuwa rafiki yake kuwa
alimwibia Diamond wake kabla hawajamwagana na kurejea tena mikononi
mwake
No comments:
Post a Comment