15 January 2015

DAZ BABA AFUNGUKA KUHUSU TUHUMA ZA MATUMIZI YA MADAWA YA KULEVYA!



Wiki iliyopita, picha ya msanii wa kitambo Daz Baba ilisambaa kwenye mitandao kama moto unaounguza msitu huku kila mmoja akitoa moani yake juu ya picha hiyo, wengine wakidai anatumia madawa ya kulevya huku wengine wakidai anaumwa kiasi cha kumuombea msaada kwa watanzania.

Nilijaribu kumcheki kupitia simu yake ya mkononi, nilimpata na akaniambia yupo Dodoma anafanya show zake, lakini zaidi ameongea leo hii juu ya lawama zote."Bwana mimi naona ni kama uzushi flani hivi kwa sababu nini nikwambie kitu, hiyo picha waliyopiga ni washkaji wa palepale Morogoro na walifanya vile kutokana na mtu aliyewatuma waje kuharibu maisha yangu ya music, kwa hiyo ndio hivyo wakafanikiwa kuiweka hiyo picha na kui-edit edit na kusema mi kichaa au naumwa sana au nahitaji msaada sijui, lakini naomba mashabiki wangu waelewa Daz Baba nipo fresh na hizo story mi huwa sirudi nyuma nimezoea kuskia story zao za uzushi uzushi tu, ila nilishawaambia wasihukumu ila naona wanaendelea kuhukumu, mi namuachia mungu ambae amenipa nguvu......."amesema Daz Baba.

"Hizo story zimeanza miaka mingi sana, kutokana na kwamba mi ni rasta fari halafu rasta fari na unga ni vitu viwili tofauti mi naishi katika misingi ya familia ya kitanzania......ujue maisha ya kujikweza mi siwezi...... lakini mi sivuti unga mimi ni rasta fari na ninaishi katika misingi ya ki rasta fari.....sipendi uzushi uzushi ........." aliendelea kusema Daz Baba.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname