Imethibitishwa kuwa nyota wa filamu nchini Nigeria, Muna Obiekwe amefariki dunia.
Kwa mujibu wa mtandao wa Tentonline, ambao asubuhi ya leo saa 12 umevunja ukimya uliokuwa umetanda kuhusu kifo cha staa huyo toka Nollywood Muna Obiekwe ambaye alifariki dunia jana mchana katika hospitali ya Festac iliyopo mjini Lagos nchini Nigeria.
Muna Obiekwe alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa ini kwa muda mrefu, ugonjwa ambao alifanya siri hata kwa wenzake wa karibu kipindi cha uhai wake. Imefahamika kuwa hali ya afya yake ilikuwa ikidhorota siku hadi siku kitu kilichopelekea kifo chake.
Kwa mujibu wa chanzo kilichozungumza kuhusu kifo cha staa huyo ni kwamba Muna Obiekwe alikimbizwa hospitali jana asubuhi baada ya kukutwa akitapika mfululizo nyumbani kwake lakini punde tu baada ya kufikishwa hospitali aliaga dunia.
Ni huzuni na pigo kwa washirika wa Nollywood pamoja na wapenzi wa filamu zake duniani kote. Mwenyezi Mungu alilaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Amen!
No comments:
Post a Comment