Yasmin Eleby hakupata mchumba wa kumuoa mtu ambaye alitaka awe mume
wake atakapofikisha miaka 40--kwa hivyo akafanya kitendo ambacho
kimewashangaza wengi, aliamua kujioa mwenyewe.
Kwa mujibu wa mtandao wa MySanAntonio.com,Eleby
aliahidi kwamba ikiwa hatapata mchumba wakati atakapokuwa ametimiza
miaka 40, basi atafanya harusi ya mtu mmoja yaani atajioa ili
kusherehekea miaka yake 40.
Duru zinasema kuwa mwanamke Eleby alifanya harusi yake mwenyewe katika
makavazi ya Houston akiambatana na jamaa na familia yake na wageni
wengine waalikwa.
Kwa sherehe hii, dadake Eleby ndiye aliendesha sherehe hio, kwani ni
kinyume na sheria kwa mtu kujioa mwenyewe. Harusi ya kawaida ni kati ya
watu wawili.
Katika picha za kanisani sherehe ilionekana kuwa ya kawaida bila ya mchumba.
Kulingana na John Guess Jr afisaa mkuu wa makavazi hayo, sherehe hiyo
ilionekana kuwa bila tashwishi na kuonekana kama jambo la kawaida kwani
makavazi hayo huwakumbatia watu wa jinsia mbali mbali kuendesha harusi
zao hapo.
Aliposikia kwamba Eleby, ambaye anaishi na kufanya kazi ugenini alikuwa
anapanga kujioa mwenyewe, aliharakisha kwenda katika eneo hilo kujionea
mwenyewe.
"Eleby alipofikisha umri wa miaka 40 bila ya kupata mpenzi na mtu mwenye nia ya kumuoa, aliamua angejioa mwenyewe,''alisema Guess Jr ambaye anasema harusi hiyo imewashangaza wengi na kuwa gumzo katika mitandao ya kijamii.
Anasema anakubaliana na Eleby na mtazamo wake wa mapenzi kwamba mtu
anaweza kujipenda na kujioa kwa kukosa wa kumuoa kwani cha muhimu ni mtu
kujipenda kwanza kabla ya kupendwa.
"watu wengu huolewa bila ya kutafakari mara mbili kuhusu yule anayemuoa, '' Guess Jr alisema.
Anadhani kwamba pindi watu watakapomuona Eleby anavyojishughulikia mwenyewe, huenda akapata ushindani. "ni mrembo, anafanya kazi kwa bidii na anasifika duniani na pia anaona uamuzi wake umewapa gumzo watu wengi.




No comments:
Post a Comment