Costa anapewa nafasi finyu ya kucheza mchezo huo, kufuatia hatua ya kufunguliwa mashtaka na chama cha soka nchini England FA, kwa makosa ya kumkanyaga beki kutoka nchini Slovakia, Martin Skrtel wakati wa mchezo wa mkondo wa pili wa nusu fainali ya kombe la ligi ambapo Liverpool walikubali kufungwa bao moja kwa sifuri.
Mshambuliaji huyo mzaliwa wa nchini Brazil, pia alionekana akimkanyaga kiungo kutoka nchini Ujerumani, Emre Can wakati wa mchezo huo lakini muamuzi Michael Oliver aliyechezesha mchezo kati ya Chelsea dhidi ya Liverpool hakuona makosa yote mawili.
FA wamejiridhisha kufanyika kwa makosa hayo mawili kupitia picha za televisheni ambazo zinaonyesha namna Diego Costa alivyowakanyaka kwa nyakati tofauti wachezaji hao wawili wa klabu ya Liverpool.
Endapo Diego Costa atakutwa na hatia kufuatia makosa hayo, huenda akafungiwa kucheza michezo mitatu iliyo chini ya chama cha soka nchini England, hali ambayo inachukuliwa kama pigo ambalo litawakuta Chelsea ambao kwa kipindi hiki wanamuhitaji kutokana na mbio za kuufukuzia ubingwa.
FA wamempa muda hadi jioni yah ii leo, mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26, kuwasilisha utetezi wake.
Wakati huo huo chama cha soka nchini Engalnd kimetoza faini ya paund 25,000 meneja wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho baada ya kumkuta na hatia kutoa kauli ya utovu wa nidhamu.
FA wamejiridhisha na kumuadhibu meneja huyo kutoka nchini Ureno, baada ya kusikia kauli yake aliyoitoa mara baada ya mchezo wa ligi kuu ya soka nchini England dhidi ya Southampton uliochezea disemba 28 haikua na tija zaidi ya kubomoa.
Mourinho alidai kwamba muamuzi aliyechezesha mchezo huo alikua na makusudi yake binafsi ya kuona wanashindwa kufanya vyema, baada ya kushindwa kutoa maamuzi ya kupigwa mkwaji wa pnati kufuatia kiungo kutoka nchini Hispania Cesc Fabregas kuangushwa katika eneo la hatari
No comments:
Post a Comment