Wakina mama, Tabu Mohamed na Mwajuma Chota ( katikati ) wakisutana kwa kuibiana mabwana.
Stori: Dustan Shekidele, Morogoro
Makubwa! Wakati Wizara ya Nishati na Madini ikiwa kwenye msukosuko wa fedha zilizochotwa ‘kihuni’ kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow, mwanaume mmoja, mtumishi wa wizara hiyo mkoani hapa almaarufu Kigogo wa Escrow, amesababisha wanawake wawili kusutana kwa matarumbeta na kukabana wakidaiwa kumgombea kwani ana fedha ‘chafu’.Tukio hilo la aina yake lilijiri wikiendi iliyopita katika Mtaa wa Karume mjini hapa ambapo wanawake hao, Tabu Mohamed na Mwajuma Chota walisababisha pakachimbika hadi polisi walipofika na kuokoa jahazi.
Awali ilifahamika kwamba wanawake hao walikuwa wakiishi pamoja maeneo ya Kikundi, Kata ya Sultan Area mkoani hapa. Kwa mujibu wa madai ya mashuhuda waliokuwa wamefunga mtaa huo, Tabu ndiye aliyeanza ‘kuchepuka’ na kigogo huyo ambaye ni mume wa mtu aliyemnunulia gari aina ya Toyota Opa.
Madai yaliendelea kushushwa kwamba, Mwajuma ambaye ni mke wa mtu alipoona mwenzake anakula vinono, naye akajiweka.SOMA ZAIDI>>>
No comments:
Post a Comment