30 December 2014

WAFAHAMU MASTAA 6 WALIOTUTOA KIMASOMASO KIMATAIFA 2014


Diamond PlatnumzMakala: Chande Abdallah
WAKATI tukimaliza mwaka 2014, wengi tunakumbuka matukio mbalimbali ya kusikitisha na machache ya kufurahisha, kama Watanzania tunapaswa kufurahia na kuwasapoti mastaa wachache waliofanikiwa kututangaza kimataifa kupitia fani na kazi zao. Wafuatao ni miongoni mwa mastaa hao:

Idris Sultan. Diamond Platnumz
Jamaa kupitia nyimbo zake amefanikiwa kutwaa tuzo tano za kimataifa kiasi cha kuitangaza nchi yake ndani na nje ya bara la Afrika. Tuzo hizo ni pamoja na tatu za Channel O Africa Music Awards (CHOAMVA) alizozitwaa huko Sauzi kupitia wimbo wake wa ‘My Number One’ aliofanya kolabo na mwanamuziki wa Nigeria, Davido. Tuzo ni tuzo za Future Music Awards ya Nigeria na nyingine ni Reggae & World Music Awards aliyoipata nchini Marekani.


Dk. Jakaya Mrisho Kikwete. Idris Sultan
Jamaa hakuwa na jina sana, lakini taratibu alianza kupata umaarufu baada ya kuingia katika mashindano ya Big Brother Africa 2014 ambapo mwishowe aliibuka mshindi wa mashindano hayo akiwapiku washiriki wenzake wengi kutoka nchi mbalimbali za Afrika. Idris aliyejizolea kitita cha shilingi milioni 510 ameingia katika listi ya mastaa waliotutoa kimasomaso mwaka huu baada ya mara kadhaa akiwa ndani ya jumba hilo kuonesha uzalendo wake wa dhati kwa nchi yake kiasi cha wengi kuitambua Tanzania.

Happiness Watimanywa. Happiness Watimanywa
Ni Miss Tanzania 2013 ambaye alituwakilisha kwenye mashindano ya dunia yaliyofanyika mwaka huu Afrika Kusini. Pamoja na kutoshinda taji hilo, Happiness anaingia katika listi ya mastaa waliotupatia sifa Watanzania baada ya kufikia hatua ya kushiriki shindano hilo bila kupata sapoti yoyote kutoka Kamati ya Miss Tanzania. Mbali na kujitoa huko miss huyo anatajwa kama mrembo aliyekubalika sana nchini kwa kupigiwa kura nyingi zaidi na Watanzania kupitia mitandao ya kijamii.

Dk. Reginald Mengi. Timothy Conrad
Muongozaji huyu wa filamu Bongo kupitia Kampuni ya Timamu African Media, ameshinda Tuzo ya Mashindano ya Silicon Valley African Film Awards zilizotolewa nchini Marekani kupitia filamu aliyoiongoza ya Dogo Masai. Timothy alishinda tuzo hiyo kupitia kipengele cha Filamu Bora ya Afrika.

Timothy Conrad. Dk. Reginald Mengi
Ni Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP. Kupitia biashara na makampuni yake amepata Tuzo ya Mafanikio ya Kutukuka, Africa Business Leadership Awards (ABBLA) iliyotolewa nchini Afrika Kusini ikiwa ni baada ya kufanya vyema katika kutekeleza maono ya kibiashara katika Bara la Afrika na kuonesha ujasiri katika kuwezesha mafanikio.

Dk. Jakaya Mrisho Kikwete
Mheshimiwa rais anafunga listi ya mastaa waliotutoa kimasomaso nchini baada ya kupokea tuzo ya uongozi bora Afrika kutoka nchini Marekani, ambako aliwakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe. Rais alitunukiwa tuzo hiyo kufuatia mchango mkubwa alioutoa kwa maendeleo ya Tanzania na Bara la Afrika kwa jumla.

1 comment:

  1. niên thư sinh một cái, không nói gì, một bên tai được Ti Đồ Nam truyền

    âm tới không nhanh không chậm.

    - Tiểu oa nhi này có chút ý tứ, thuật xem tướng cũng có chút thủ đoạn, nhưng đấy là đối với người bình thường thôi. Còn đối với những người tu
    dịch vụ kế toán thuế trọn gói
    trung tâm kế toán tại tphcm
    ngoduong
    học kế toán tại cầu giấy
    kế toán cho giám đốc
    chung cư newskyline văn quán
    chung cư goldmark city
    dịch vụ kế toán trọn gói
    học kế toán phần mềm misa
    học kế toán thực hành
    meomeo007 01embesexy
    trung tâm kế toán tại hà đông
    chung cư hà nội
    trung tâm kế toán tại thanh xuân
    dịch vụ kế toán thuế
    dịch vụ báo cáo tài chính

    tiên chúng ta thì đúng là mua búa trước cửa Lỗ Ban, lão phu đem cảnh

    giết người diệt mônt rước kia truyền vào trong trí nhớ hắn một lần. Hắc

    hắc, cũng nên làm cho hắn không tiệu thụ được một chút.

    Chỉ trong chốc lát trung niên thư sinh lập tức xuất hạt mồ hôi đầm đìa, ánh mắt nhìn về phía Vương Lâm không còn bình thản như lúc đầu nữa. Lúc

    này đã lộ ra vẻ kính sợ, hắn nghe được lời Liễu Tam nói vội vàng khoát

    tay:

    - Tiểu.... huynh đệ này không có quan hệ, tiểu huynh đệ ngày sau tiền đồ

    vô lượng. Vương mỗ đối với thuật xem tướng không tinh thông, không thể

    nhìn thấu.... không thể nhìn thấu....

    Nói xong, hắn cuống quít chắp tay thi lễ, vẻ mặt vô cùng đau khổ.

    ReplyDelete

Comments system

Disqus Shortname