04 December 2014

MAASKOFU WA ESCROW! KILAINI, NZIGIRWA, TWIMANNYE NITAUNGAMA NIKIWATAZAMA USONI

Baba Askofu Methodius Kilaini akitoa huduma kanisani. UKIHOJI dhambi za viongozi wa dini harakaharaka utaambiwa fuata mafundisho yao usifuate matendo. Hili ni kinyume na Mtume Paul aliyefundisha waumini wake kuwa wamfuate yeye kama alivyomfuata Yesu. 

Kwa kuwa dini ni muhimu kwenye kaya yangu sibishi sana katika hilo, lakini kuhusishwa kwenye fedha chafu kwa viongozi wa dini Askofu Methodius Kilaini, Euesebius Nzigirwa na Alphonce Twimannye kumenibadilisha mtazamo. 
Sikuwahi kuuliza utakatifu wa viongozi hao wa dini kwa sababu za kutofuata matendo yao; lakini sakata la ufisadi wa Escrow wa zaidi ya shilingi bilioni 300 limenifanya nijiulize kimoyomoyo watawa hawa walipewa fedha hizo kwa ajili ya kazi gani?
Swali hili lipo na litaendelea kuwepo kwa sababu Mkuu wa Kaya sijapata majibu ya msingi. Kwa hali hiyo, hata nitakapokwenda kuungama dhambi zangu mbele ya watumishi hao wa Mungu nitakuwa nawatazama usoni. 

Ukweli ni huo; nitakuwa natubu dhambi zangu lakini wakati huohuo nayauliza mapaji ya uso ya viongozi hao kulikoni wakajichotea mamilioni ya fedha ambazo hazina utakaso? Nitafanya hivyo kwa sababu utetezi unaoenezwa juu ya watawa hao kuhusu kupewa fedha za Escrow haujanikata kiu. Nafikiri siyo mimi tu, ni pamoja na wanazengo wenzangu katika kaya hii.Askofu Euesebius Nzigirwa(wa pili kulia) akiingia kanisani. SOMA ZAIDI>>>

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname