01 December 2014

HUYU NDIYE SINGASINGA TAPELI WA ESCROW



Harbinder ambaye ni singasinga anatajwa pia akidaiwa kuwa mfanyabiashara tapeli kufuatia vitendo vyake mbalimbali katika kumiliki makampuni na ukwepaji wa kodi ya serikali.Unamjua? Anaitwa Harbinder Singh Sethi! Ni mfanyabiashara bilionea mwenye asili ya Bara la Asia na mmiliki wa mtambo wa kufua umeme wa Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) ambayo hivi karibuni imezua tafrani Bongo kufuatia kampuni yake kuhusishwa na uchotwaji wa fedha kiasi cha Sh. Bilioni 306 kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
HISTORIA YAKE FUPI
Harbinder anatajwa na vyanzo kwamba ni mzaliwa wa Mkoa wa Iringa. Mwaka 1977 akiwa na umri wa miaka 20 ya kuzaliwa na nduguze wawili, Nota Singh na Manjit Singh walianzisha kampuni ya ujenzi wa barabara iliyojulikana kwa jina la Ruaha Concrete Co. Ltd ikitumia SLP 498, Iringa. Ruaha ni sehemu maarufu kwenye Manispaa ya Mji wa Iringa kukiwa na vitongoji vya Ipogoro, Kibwabwa na Ndiuka. Jina la Ruaha linatokana na Mto Ruaha kupita eneo hilo. 

Vyanzo vinasema, Harbinder alianza kumiliki fedha nyingi kuanzia miaka ya 80 wakati familia ya Rais wa Kenya wakati huo, Daniel Arap Moi ilipoanza kujiingiza kwenye biashara mbalimbali.SOMA ZAIDI>>>

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname