Tumekaa na Diamond Platnumz kuzunguma mambo kibao hususan tetesi zinazoendelea sasa kuwa ameachana na mpenzi wake Wema Sepetu na kuwa ana uhusiano na mfanyabiashara mrembo wa Uganda, Zari the Bosslady pamoja na issue zingine. Itazame hapo chini au soma kwa kifupi baadhi ya kile Kuhusu kwanini anatumia wazungu zaidi kwenye video zake Mimi nafikiri ni kutokuwa na uelewa tu kwasababu inategema na concept. Ukiangalia kama ‘Mdogo Mdogo’ ilikuwa inazungumzia mapenzi hayaulizi kwanini so ilikuwa lazima ioneshe pande mbili, kuna wazungu na mimi ni mwaafrika na familia yangu ya kiafrika. Kuna mtoto wa kizungu ambaye ananizimia mimi mwaafrika lakini familia yake haipendi ukizingatia wao ni wafalme na nini. Lakini mtoto bado ananipenda hivyo hivyo, ananifuata mpaka porini ananikuta kwenye maji naimba mimi kule. Mpaka dakika ya mwisho anakuja baba yake anamkuta yupo kwetu kijijini anacheza na familia yetu sisi so dakika ya mwisho unakuta mzee mwenye anakubali mwanae aolewe.
Sasa huwezi kufanya familia ya kiafrika na familia ya kiafrika, haiwezi kuleta maana, lazima iwe tofauti. Ukiangalia kama video ya ‘Ntampata Wapi’ watu wanashindwa kuelewa, yule model sio mzungu. Ni mwaafrika sababu anaishi south kaiva sana. Ukiangalia kuna waafrika, kuna wazungu.. unajua ukiwachanganya inakufanya uweze kuwavuta na watu wengine waconcentrate na ile nyimbo, waone kama hata sisi inatuhusu, usifanye issue za kibaguzi.
Kuhusu anavyomchukulia model wa kwenye video ya Ntampata Wapi, Melissa
Kiukweli amejitahidi na amefanya vizuri sana. Bado tunawasiliana, hata juzi nilimtumia meseji nikamwambia ‘Melissa natamani ujue jinsi gani unazungumziwa, nikasema ‘najua kabisa huko South Africa hawawezi kuwa wanaizungumzia hii video kama wanavyoizungumzia hii video huku nyumbani, natamani ujue jinsi gani walivyokupokea, natamani ujue umefahamika kiasi gani.BOFYA KUONA VIDEO YA MAOJIANO YA DIAMOND>>>
No comments:
Post a Comment