Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili, baadhi ya wananchi wamesema mtu akitaka riziki kirahisi ajiingize katika siasa na kuanza kuihubiri pia aondoe woga kama washiriki katika sakata hilo walivyofanya kwa kujipa ujasiri wa kujichotea shilingi bilioni 306 kutoka kwenye akaunti hiyo.
ISIKIE HII
“Sasa nimeamini, ukitaka kuwa tajiri mkubwa katika nchi hii, we eneza siasa, utaweza kuchota riziki (pesa) kubwa sana hususan kama utaondoa woga,”
alisema Fred Jimmy ‘Fredwaa’, mkazi wa Makumbusho jijini Dar es Salaam.
Pamoja na yote hayo, wananchi hao wamesema chochote kitakachofanyika, ni lazima fedha hizo zirejeshwe kutoka kwa wahusika hao, kwani ni fedha za walipa kodi wa Tanzania ambao maisha yao ya kila siku ni ya kubangaiza.
Askofu Mkuu Msaidizi Jimbo la Kagera, Methodius Kilaini.
“Ripoti ya PAC tumeiona na utetezi wa Waziri Sospeter Muhongo pia tumeusikia, lakini hatuukubali. Anadai kuwa Tanesco haina fedha kwa kuwa haijaanza kutengeneza faida, kwamba kwa muda wote imekuwa ikidaiwa tu.
“Sawa, hatukatai Tanesco inadaiwa (bilioni 90 na capacity charge’) lakini si ni kweli pia kwamba Tanesco hiyohiyo ilikuwa inaweka yale mabilioni kwenye ile akaunti ya Escrow?” alihoji mwananchi mmoja aliyejitambulisha kama Justin Sompa, mfanyakazi serikalini jijini Dar es Salaam.
Akaendelea: “Kwa hiyo kwa akili ya kawaida, madeni yanayodaiwa Tanesco hayana uhusiano na fedha za Escrow na ukweli unabaki kuwa kwenye Kamati ya Zitto (PAC), hizi pesa zinatakiwa zirudi mara moja na waliohusika lazima wapandishwe kizimbani na ikibidi wafilisiwe mali zao.”SOMA ZAIDI>>>>
No comments:
Post a Comment