MATOLA (KUSHOTO), AKIMUONYESHA SAA KIUNGO KISIGA, KWAMBA AMECHELEWA. KATIKA NI MENEJA WA SIMBA, NICO NYAGAWA. |
Kocha Msaidizi wa Simba, Selemani Matola ameonyesha hataki kuchukuliwa
‘poa’ baada ya kumkomalia kiungo Shabani Kisiga na kumtimua mazoezini.
Matola alimfukuza Kisiga mazoezini wakati wakiwa kwenye gym ya Chang’ombe.
Wachezaji wote walikuwa wamefika siku hiyo na Kisiga akachelewa kwa nusu saa.
Matola akasisitiza suala la nidhamu na hasa kwa Kisiga ambaye ni mkongwe.
Usisahau, tayari Kisiga alikuwa ametoka kwenye kesi.
Lakini
hakuwa na ujanja zaidi, zaidi ya kuondoka kwa kuwa msimamo wa Matola
ulibaki palepale, kwamba kila mchezaji lazima ajali muda.
No comments:
Post a Comment