Aliyekuwa Miss Tanzania 2014 Sitti Abbas Mtemvu.
HAIJAKAA sawasawa! Siku chache baada ya Sitti Abbas Mtemvu (25) kujivua taji la Miss Tanzania 2014 kwa madai ya kusakamwa na vyombo vya habari kuhusu umri wake, wadau wamemwangushia uwajibikaji mwingine wakimtaka avue mataji mengine mawili.Baadhi ya wadau wa sanaa waliozungumza na Risasi Mchanganyiko Jumatatu iliyopita jijini Dar walisema kama kweli Sitti ana dhamira safi ya kukwepa kusakamwa basi ni bora kwake akavua na mataji ya Miss Chang’ombe na Miss Temeke ambayo ndiyo yaliyompa tiketi ya kwenda kambi ya Miss Tanzania na kushinda.
Wadau hao walisema kuwa, sheria za Miss Tanzania zinaanzia vitongojini, wilaya, mikoa, kanda na hatimaye taifa kwa hiyo kama skendo ya kudanganya umri imemla mpaka akaamua kujisalimisha, basi bado hana sifa za kuwa Miss Chang’ombe na Miss Temeke wa mwaka 2014.
“Kwanza kabisa nasema Sitti hajavua taji la Miss Tanzania kwa sababu ya kusakamwa na vyombo vya habari kuhusu kudanganya umri bali ni kweli amedanganya, anajijua.INAENDELEA>>>
No comments:
Post a Comment