Baba huyo akizuiwa ili asiendelee kushusha kichapo hicho. Kwa mujibu wa mashuhuda wetu, tukio hilo lilijiri juzikati, maeneo ya Mwananyamala-Komakoma jijini Dar ambapo awali binti huyo ambaye ni msanii chipukizi wa kuigiza aitwaye Jeniffer alidaiwa kupigwa mkwara na baba yake kuwa asijishughulishe na masuala ya muvi na badala yake ajikite kwenye masomo yake kufuatia tasnia hiyo kuhusishwa na skendo za ngono.
Ilidaiwa kwamba, Jeniffer alikaidi amri ya mzee wake huyo na kwenda kinyemela kurekodi vipande kadhaa vya muvi ya kikundi chao ambapo taarifa zilimfikia baba yake huyo na kuamua kutimba lokesheni.
Baba huyo akijiandaa kumvaa prodyuza huyo. Ilisemekana kwamba, katika hali iliyompandisha zaidi hasira, mzee huyo alipofika maeneo hayo alimkuta mwanaye katikati ya ‘scene’ ya mahaba aliyokuwa akiigiza na msanii anayetamba kwenye Tamthiliya ya Siri ya Mtungi, Daudi Michael almaarufu Duma.
No comments:
Post a Comment