Saa ghali zaidi duniani imenunuliwa mnadani huko Geneva,Uswiss kwa gharama ya dola za kimarekani milioni 21.3.
Saa
hiyo imetengenezwa kwa kutumia karati ishirini na moja za dhahabu na
ina uzito wa nusu kilo,saa hiyo iliyoundwa kwa mbwembwe ilitengenezwa
mahsusi kwa ajili ya mtoto wa mfanya biashara,Henry Graves mnamo mwaka
1930.Na ilimchukua miaka nane kwa watengeneza saa maarufu wa Uswis kuikamilisha hiyo saa ghali ambaye ni Patek Philippe.
Saa hiyo ilinunuliwa siku mbili tu baada ya mmiliki wa mwisho kufariki dunia kutoka falme za kiarabu Saud Bin Mohammed Al-Thani.
Mmiliki huyo alikuwa na madeni mengi ambayo yangemgharimu nyumba yake kuuzwa na hivyo akaikabidhi saa hiyo kwenye nyumba ya mnada ya Sothebys.
No comments:
Post a Comment