11 November 2014

NATESEKA..!!! NILIJUA NI MIMBA KUMBE NI UGONJWA

Flora Samweli Luvinga (24) anyesumbuliwa na uvimbe mkubwa tumboni.

Mgonjwa huyo ambaye kuumwa kwake kumechukua muda mrefu bila mabadiliko ya kupata nafuu, afya yake imezidi kudhoofu jambo lililomfanya mama yake mzazi kupatwa na presha siku za hivi karibuni na kufariki dunia baada ya kushindwa kupata fedha kwa ajili ya kumtibia.
Katika mahojiano na mwandishi wa habari hii wiki iliyopita saa chache baada ya kurejea jijini Dar akitokea Iringa, Flora aliyekutwa amekaa chini maeneo ya Mwenge akipumzika kutokana na maumivu makali, alikuwa na haya ya kusema:

Mama mmoja mkazi wa Kijiji cha Kipanga, Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa, Flora Samweli Luvinga (24) hali yake ipo hatari baada ya kuvimba tumbo na kumsababishia maumivi makali.“Awali nilidhani ni mimba baadaye nikajua kuwa kumbe siyo bali ni ugonjwa ambao unanipa mateso kwa muda mrefu, sasa sijui hatima ya maisha yangu hapa duniani,” alisema Flora.“Siamini kama ipo siku nitapona na kurejea hali yangu ya kawaida, hapa nilipofikia nimekata tamaa, kwani nimehangaika kwa muda mrefu katika matibabu bila kupata nafuu.INAENDELEA>>>

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname