08 November 2014

MZEE WA UPAKO ASAKWA, ADAIWA KUTISHA KUMUUA MUUMINI WA GWAJIMA!

Kijana anayejitambulisha kwa jina la Robert Lugala, anayedai kutishiwa maisha na Mchungaji Lusekelo Anthon. Akizungumza na waandishi wetu juzi jijini Dar, Robert ambaye shughuli zake ni kuuza chipsi usiku kucha, alisema mara kwa mara Mzee wa Upako amekuwa akimfuata eneo lake la kazi na kumtishia maisha kwa kumwambia maneno mbalimbali yenye vitisho.
“Mara ya kwanza ilikuwa Oktoba 9, mwaka huu saa kumi kasoro usiku. Alipaki gari lake, Land Cruiser (Toyota) nyeusi.
LILE sakata la Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) Ubungo – Kibangu, Dar, Lusekelo Anthon ‘Mzee wa Upako’ kufyatua risasi mtaani limechukua sura mpya baada ya kijana aliyejitambulisha kwa jina la Robert Lugala, mkazi wa Kibangu kuibuka na kudai alitishiwa kuuawa kwa kupigwa risasi na mchungaji huyo
Akaniangalia na kuniambia nina macho makali. Akasema ataniombea nitaanguka. Nikamkatalia na kumwambia mimi nina nguvu za Mungu wa kweli, nasali kwa Gwajima kwa hiyo siwezi kuanguka. Aliposhindwa akaahidi kurejea siku nyingine.
“Mara ya pili ni Oktoba 13, mwaka huu saa nne usiku alikuja tena. Mara ya tatu ni Oktoba 15 saa kumi usiku akaanza kugawa pesa kwa madereva wa bodaboda huku akiwaamrisha kuniimbia nyimbo ya kunilaani. Kweli waliniimbia.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname