17 November 2014

MADAI MAZITO: BODABODA ACHINJWA KIKATILI KWENYE FUMANIZI MKOANI MOROGORO!


Marehemu Kambi enzi za uhai wake. Tukio hilo lilitokea juzikati majira ya saa 11:00 alfajiri ambapo mwili wa bodaboda huyo uliokotwa maeneo ya Modeko jirani na Makutano ya Barabara za lringa na Mazimbu na kusababisha mkewe kuchanganyikiwa huku ndugu wakiwa hawaamini.
HATARI! Wimbi la mauaji yanayohusishwa na matukio ya mafumanizi yanazidi kushika kasi mkoani hapa ambapo mwishoni mwa wiki iliyopita dereva mwingine wa bodaboda aliyetajwa kwa jina moja la Kambi (33), anadaiwa kuchinjwa na kufa papohapo huku kifo chake kikihusishwa na matukio hayo.

Mke wa marehemu akiwa mwenye huzuni kubwa.Muda mfupi baada ya tukio hilo, mwanahabari wetu alifika eneo la tukio na kuushuhudia mwili wa jamaa huyo ukiwa umetupwa lakini hawakuchukua chochote kutoka kwa marehemu huku wakimwachia bodaboda yake na waleti ikiwa na fedha taslimu shilingi laki 240,000.SOMA ZAIDI>>>

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname