08 November 2014
CHUCHU WA RAY AZUA TIMBWILI BARABARANI!
Baby wa Vincent Kigosi ‘Ray’, Chuchu Hancy. Timbwili hilo lilitokea juzikati maeneo ya Kinondoni jijini Dar ambapo msichana huyo alikuwa akiendesha gari hilo aina ya Mark X nyeusi ambalo limefanana na la Ray, Chuchu alipoliona kwa mbali linaendeshwa na msichana, akaanza kulikimbiza.
NI mkalia nyonga wa Vincent Kigosi ‘Ray’, Chuchu Hancy amezua timbwili la aina yake barabarani baada ya kukimbiza gari la msanii aitwaye Ester Kiama akijua ni gari la ‘bebi’ wake.
Chanzo kilichoshuhudia ishu hiyo kimesema licha ya Chuchu kufanikiwa kulipata na ‘kuliziba’ kwa mbele gari hilo, aliumbuka pale alipolikagua na kugundua si la Ray.Alipoulizwa Chuchu na mwanahabari wetu kuhusu tukio hilo, alijibu kwa kifupi:
“Jamani naomba hilo sipendi kulizungumzia.”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment