
Msanii
wa filamu nchini Irene Uwoya amefunguka leo katika blog hii... na
kusema kuwa yeye hajaachana na mumeo wa ndoa na wala msanii Diamond
Platnum hajavunja ndoa yao kama ambavyo baadhi ya watu na vyombo vya
habari walivyokuwa wakisema.Uwoya ameweka wazi suala hilo baada ya
mashabiki wengi
kutaka kujua kama ameachana na mumeo ndikumana na ndipo hapo amekanusha
kuwa hajawahi kuwa na mahusiano na Diamond Platnum wala Msanii Msami
Baby kama ambavyo watu wamekuwa wakijua ni wapenzi bali amesema kuwa
yeye na msanii Msami ni marafiki wa karibu na sasa wanafanya filamu ya
pamoja.
Gasper
Nataly :una mahusiano ya kimapenzi na Msanii Msami >>> Irene
Uwoya: hapana Donlee Guck i love my sister,unachukuliaje skendo za wa
sanii bongo?,kwanini uliamua kuachana na Mr
Ndikumana>>>>>Irene Uwoya kawaida hatujaachana SINA BIFU
NA JACKLINE WOLPER Kuna wakati uvumi ulienea kuwa Irene Uwoya amekuwa na
bifu na msanii mwenzake wa Filamu Jackline Wolper lakini leo kupitia
Kikaangoni Live Irene Uwoya amekana kuwa na bifu na Wolper na kudai kuwa
Jackline ni mtu wake wa karibu ambae amekuwa akimshirikisha katika
mambo mbalimbali hali ambayo anamfanya ajione ni kama pacha wake
kutokana na kuelewana na kushabiana katika mambo mbalimbali. Tuma Simba
Ni kweli bifu lenu ww na jacline wolper limemaliza?
>>>>>>Irene
Uwoya hatuna bifu na pacha wangu Wolper. SIWEZI KUVAA NGUO NDEFU Uwoya
ambaye huwa ni hatari sana akiwa katika kazi yake ya uigizaji hususani
zile scene za mahaba niuwe amesema kuwa katika maisha yake ya kawaida
mbali na uigizaji amekuwa akizichukia na kutozipenda nguo ndefu hiyo
ndiyo sababu inayomfanya kuvaa nguo fupi katika kuigiza hata katika
maisha yake ya kawaida.Elizabeth Kisiri dada Irene kama nitakua
nimekukera nisamehe ivi kwanini huwa unapenda kuvaa nguo fupi mfano wa
nguo ya klabu una akiwa unaigiza scene za ofisini?kwanini dada yangu
wakati ofisini unatakiwa kuvaa suti au nguo yoyote ya heshima?
>>>>>>>Irene
Uwoya nimezoea tu na napenda pia nguo fupi ndio maana siwezi kuvaa
ndefu,maana nikivaa nguo ndefu nakereka,naweza kusema kuwa nina areji na
nguo ndefu. MZEE MAJUTO NA JB KIBOKO Uwoya amesema kuwa katika kufanya
kazi na wasaniii mbalimbali amekuwa akipenda sana kufanya kazi na mzee
Majuto na Jb maana wanajua wanachokifanya katika kazi pia ndio watu
ambao yeye amekuwa akiwapenda na kuwakubali katika tasnia ya filamu kwa
Tanzania. Mudy Santos Ni msanii gan wa kiume anaependa kuigiza nae?
No comments:
Post a Comment