23 October 2014

WEMA SEPETU: WAKATI BEBI WAKE AGIUGULIA MAUMIVU,


WAKATI bebi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiugulia maumivu ya kuzomewa na mamia ya mashabiki wa muziki katika Tamasha la Fiesta jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wikiendi iliyopita, Wema Sepetu ‘Madam’ anaponda raha ya maisha nchini China, Amani lina full data.Bebi wa mbongo Fleva ‘Diamond Platnumz’ , Wema Sepetu ‘Madam’. Chanzo makini kilicho ‘kloz’ na muigizaji huyo nyota wa filamu nchini, kimesema Wema alipaa na ndege ya Emirates wiki iliyopita, siku chache kabla ya Tamasha la Fiesta, akiwa
ameandamana na wanaume wawili, ambao ni meneja wake, Martin Kadinda na Petit Man, wote wakiwa wamekaa daraja la kwanza la dege hilo. Chanzo hicho kilizidi kunyetisha kuwa gharama zote za safari hiyo zilibebwa na Madam mwenyewe na kwamba baada ya kufika katika jiji la Guangzhou nchini humo, Wema na wanaume hao wawili walichukua vyumba katika Hoteli ya Holiday Inn, inayotajwa kuwa moja ya hoteli ghali zaidi huko China. 

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname