23 October 2014

VYETI VYA MISS TANZANIA 2014 VYAANZA KUCHUNGUZWA NA RITA, IKIBIDI POLISI KUHUSISHWA


WAKALA wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), imeanza uchunguzi wa vyeti vya Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu, baada ya kuibuka utata wa taarifa za kuwapo vyeti viwili vinavyotofautiana maelezo.
Uchunguzi wetu umethibitisha kuwapo upekuzi maalumu wa nyaraka alizowasilisha Sitti katika ofisi za RITA Temeke ili kubaini kwanza uhalali wa cheti, kabla ya kutafuta ukweli wa taarifa zilizowasilishwa chini ya kiapo.
Kwa mujibu wa Sheria ya Usajili wa Vizazi na Vifo (Sura ya 108 Toleo la 2002), ni kosa la jinai kutoa taarifa za uongo kwa Msajili na pia ni kosa la jinai kughushi, mambo ambayo yakithibitika RITA watalazimika kulikabidhi suala hilo kwa Jeshi la Polisi.

Mkurugenzi wa Sheria wa RITA Emmy Hudson,  amesema kuwa mamlaka hiyo inachunguza suala hilo kwa umakini ili kuhakikisha haki inatendeka kwa mhusika.SOMA ZAIDI HAPA>>>

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname