Bw. Japhet Kwangula akieleza katika Mkutano wa wakulima wa pamba uliofanyika
hivi karibuni wilayani Bunda juu ya umuhimu wa kupata pembejeo kwa wakati na
kwa kiwango kinachotakiwa. Katika mkutano huo, wakulima waliweza kupata fursa
ya kujadili ya mafanikio na changamoto zilizopo kwenye sekta ya pamba sambamba
na kujadiliana namna ya kupata njia sahihi ya kuwawezesha kufanya vizuri na
hivyo kufikia malengo kwa msimu ujao.
|
No comments:
Post a Comment