Kwa mara nyingine tena, mashabiki wa Diamond Platnumz wameshindwa kumuona akitumbuiza licha ya kumsubiria hadi saa 10 Alfajiri.
Awamu hii imetokea jijini London, Uingereza katika show aliyoitangaza kwa kiasi kikubwa kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii. Tofauti na Stuttgurt, Ujerumani ambako mashabiki walifanya uharibifu mkubwa, mashabiki wa London waliamua kuwa wapole tu na kurejea majumbani mwao na hasira walizozimeza vifuani.
Chanzo cha Diamond kutotumbuiza kwenye show hiyo kinaonekana kuwa ni kile kile kama cha Ujerumani wiki kadhaa zilizopita yaani promota kushindwa kumlipa fedha yake. Staa huyo hakuchelewa kumtupia lawama promota wa show hiyo, DJ Rule. Akiweka picha ya promota huyo kwenye Instagram, Diamond ameandika:
Tafadhari ndugu zangu wa UK!!!….kuweni makini sana na promoter huyu (Victor – Dj rule) mnaposikia kaandaa show, party au hafla yoyote…ni vyema kuziepuka na kutohudhuria kabisa kwasababu ni tapeli…. si unajua aisifiae mvua imemnyeshea… basi mie nimeloa kabisa.” Tunafanya jitihada za kumpata DJ Rule kujua upande wake.
bongo 5
No comments:
Post a Comment