Akizungumza kupitia Kipindi cha Mkasi kinachoratibiwa na Mtangazaji Salama Jabir, Jumatatu iliyopita, Nora alisema fani ya uigizaji imevamiwa kwa sasa kwani kuna watu ambao wanaingia kwenye gemu ili wauze sura na kuonekana na wanaume wapate ‘soko’ kiulaini.
Aliongeza kuwa, watu hao kupitia vitendo hivyo wamekuwa wakiichafua tasnia kiasi cha wote kuonekana hawafai (samaki mmoja akioza, ni wote).
Nora alikwenda mbali zaidi alipoulizwa na Salama ni nani na nani hawafai na nani wanafaa, alishindwa kuwataja kwa majina moja kwa moja lakini mtangazaji huyo akaomba ataje majina yeye kisha Nora aseme kama anafaa au hafai!
Salama: “Kajala.”
Nora: “Huyo hamna kitu.”
Salama: “Batuli.”
Nora: “Huyo pia hamna kitu.”
Salama: “Lulu.”
Nora: ”Huyo safi.”
Salama: “Mlela (Yusuf).”
Nora: “Huyo hamna kitu.”
Salama: “Steve Nyerere.”
Nora: “Huyo hamna kitu.”
Salama: “Hemed (Suleiman).”
Nora: “Hamna kitu hapo.”
Globalpublishers ilimsaka Kajala kwa njia ya simu hakupatikana, lakini mmoja wa watu wake wa karibu alisema staa huyo ameshangaa sana Nora kutaka kurudi juu kwa kutumia jina lake.
“Kajala amezima simu, lakini kamshangaa sana Nora, alishazimika, sasa anaonekana anataka kuwaka tena kwa kutumia jina lake,” alisema mpambe huyo.
No comments:
Post a Comment