20 September 2014

Picha: Balotelli Alipandisha Meli Gari Lake lenye Thamani ya Pound 240,000


Mshambuliaji kutoka nchini Italian Super Mario Balotelli, ameshindwa kujizuia na kulazimika kuagiza gari lake aina ya Ferrari F12 Berlinetta kutoka nchini Italia.
Balotelli, amelazimika kufanya hivyo kutokana na mazoea yaliyojengeka ya kutumia gari hilo mara kwa mara katika safari zake, tangu alipolinunua akiwa na klabu ya AC Milan kwa gharama ya Paund 240,000.
Katika hali ya kushangaza hii leo mshambuliaji huyo, alitinga kwenye uwanja wa mazoezi wa Liverpool
akiwa anaendesha gari hilo na kuwafanya waandishi wa habari kushangaa kutokana na kutoamini alichokifanya.

Sababu kubwa iliyosababisha mshangao kwa walio wengi ni kitendo cha mshambuliaji huyo kuamua kuagiza gari lake kutoka nchi ya Italia, kitendo ambacho ni tofauti na wachezaji wengi ambao huzihama klabu zao na kulazimika kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine.
Mara nyingi wachezaji wanapohama nchi hulazimika kuuza majumba yao ya kifahari pamoja na mali zao nyingine kwa ajili ya kwenda kuanzisha maisha mapya waendapo, lakini kwa Balotelli imekuwa tofauti.


Balotelli akiwasili kwenye uwanja wa mazoezi wa Liverpool mapema hii leo.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname