13 September 2014

ONYESHO LA SERENGETI FIESTA GEITA KUACHA HITORIA





Baada ya kufanikiwa kufanya onyesho kubwa na la kuvutia mjini Shinyanga jana, sasa kituo kinachofuata kwa ajili ya Serengeti Fiesta 2014 ni Geita, linalotarajiwa kufanyika leo katika ukumbi maarufu wa Desire Park.

“Kaulimbiu ya Serengeti Fiesta 2014…'Ni shiiiiida!’ sasa imegeuka kuwa msemo maarufu miongoni mwa vijana wa Mkoa wa Geita na Jumamosi hii tutathibitisha hilo kwa watu wote wa Geita,” anasema Rugambo Rodney, Meneja wa Bia ya Serengeti Premium Lager.

Matukio kadhaa kabla ya onyesho hilo na promosheni nyingi za kulipamba onyesho lenyewe linalotarajiwa kuwa la kukumbukwa tayari yamekwishaanza huku Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kupitia bia yake, Serengeti Premium Lager, kwa kushirikiana na waandaaji, Prime Time Promotions, wameahidi kutoa kile kilichobora kabisa kwa watu wa Geita.

Rodney aliendelea kusema: “Ukichukulia mafanikio tuliyoyapata Shinyanga, ni dhahiri kuwa tuna nafasi kubwa ya kufanya jambo kama hilo kwa watu wa Geita na tuna matumaini makubwa tamasha hili litakuwa ni la kukumbukwa daima.”

Shoo ya Serengeti Fiesta 2014 mjini Geita itawapandisha jukwaani wasanii maarufu wanaokubalika nchini ambao ni Christian Bella, Ommy Dimpoz,  Fareed Kuband a.k.a ‘Fid Q’, Chege na Temba, Linah, Recho, Young Killa, Ney wa Mitego pamoja na Stamina.

Mbali na shoo, shughuli nyingine nyingi zitafanyika mapema, kuanzia bonanza la soka na ‘Dance la Fiesta’ ambapo washindi mbalimbali watapewa nafasi ya kusafiri hadi Dar es Salaam kushuhudia onyesho la mwisho linalotarajia kufanyika Oktoba 18 mwaka huu.

Shoo ya Geita itakuwa ni ya saba katika ziara hii huku mikoa mingine zaidi ya 10 ikiwa kwenye dada za SBL kupelekewa simulizi hii kubwa nchini Tanzania kwa sasa.




ABOUT SERENGETI BREWERIES LIMITED 
Serengeti Breweries Limited engages in the brewing, manufacturing, marketing and selling drinks made of malt, hops and barley and sorghum in Tanzania.
 Headquartered in Dar es Salaam, SBL brands include:- Serengeti Premium Lager, Serengeti Platinum, Tusker Lager, Tusker Lite, Kibo Gold, Uhuru Peak Lager, Pilsner Lager, Senator, The Kick and Guinness®.
 SBL is also the sole distributor of several international renowned spirits including Smirnoff Vodka®, Johnnie Walker®, Bailey’s Irish Cream ®, Richot®, Bond 7 Whiskey® and Gilbeys Gin®.
 Serengeti Breweries Limited is a subsidiary of East African Breweries Limited/ DIAGEO PLC.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname