DIAMOND AWACHANA LIVE KILI MUSIC AWARDS...CHEKI ALIVYO TIRIRIKA HAPA

Well"
Nimekuwa nikipokea maswali na Comment nyingi eti kwanini sitangazi
vipengele vyangu vya Tunzo watu wanipigie kura...tafadhali naomba
mniskilize kwa umakini:
Ikiwa
MOE MUSIC hakuonekana ni Mmoja ya Mwanamuziki bora Chipukizi..
NDAGUSHIMA ya Ommy Dimpoz haikuonekana inafaa kugombea kama Moja ya
Video bora..Video ya Rich Mavocal - PACHA WANGU haikuonekana inafaa
kugombea kama moja ya video bora.... YAMOTO BAND licha ya kuvuma na
kujaza kila show ya kila pembe ya Tanzania ila Mwisho wa Siku
wameambulia Category Mbili tu Unafkiri mimi nina haja gani ya Kuomba
kura???? Hivi kuna Nyimbo zimependwa na kuvuma kama NITAJUTA ama NISEME
ya YAMOTO BAND Tanzania?? Eti mwisho wa siku, watoto wa watu licha ya
Juhudi zote eti hazikustahili wameambulia Category Mbili tu... Hivi
kweli Tunakuza Muziki wetu au Tunaua??? Mimi Kuwa na Categories 10 na
Kuongoza kuwa na Vipengele vingi kuliko Masanii yoyote hakunifanyi eti
nifurahie Wengine wanapoumizwa kwasababu kama leo wameumizwa wao basi
kesho pia nami ntaumizwa ...Pia Kwangu mimi sifanyi mziki ili Nifaidike
bali nafanya ili wasanii na Taifa langu pamoja na Tasnia yangu izidi
kufika mbali na tuheshimike... I have been to this Industry zaidi ya
Miaka Mitano (5 ) so panapo NAMNA Napajuaga mapema na Ndiomaana sitaki
kuwapotezesha watu pesa zao wanipigie kura halaf ziende na maji...
Wakiona kuna mahala nilistahili watatoa wakiona sijastahili ni haki
yangu kutopewa...Nilishawai hata kutopewa tunzo kabisa ila Mpaka leo
sijawai shuka na Sitokaa Nishuke labda Waniue!....Napost PART 2
No comments:
Post a Comment