Stori: Imelda Mtema
NI sheeda! Muigizaji wa filamu za Kibongo, Salim Omary ‘Slim’ amejikuta akiwekwa nguvuni katika Kituo cha Polisi cha Makangarawe, Yombo-Buza, jijini Dar akidaiwa kugoma kurejesha gari aina ya Land Lover Discovery walilopewa zawadi siku ya ndoa.
NI sheeda! Muigizaji wa filamu za Kibongo, Salim Omary ‘Slim’ amejikuta akiwekwa nguvuni katika Kituo cha Polisi cha Makangarawe, Yombo-Buza, jijini Dar akidaiwa kugoma kurejesha gari aina ya Land Lover Discovery walilopewa zawadi siku ya ndoa.
Gari hilo walipewa na wakwe zake alipofunga ndoa na binti yao aitwaye
Asia Morgan, mwaka jana lakini ilipofika Mei mwaka huu (takriban miezi
tisa tu ndani ya ndoa), wawili hao walitengana na kusababisha wakwe hao
wageuke mbogo kudai chao kwa maelezo kwamba walitoa zawadi hiyo kwa
binti yao hivyo kwa kuwa wametengana, wanataka chao.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Asia alifikia uamuzi wa kwenda kuishi
nyumbani kwao Tegeta, jijini Dar baada ya kushindwa kuvumilia tabia ya
wivu wa kupindukia aliyokuwa nayo Slim.
“Baada ya kutengana wazazi wa msichana huyo walimwambia Slim awakabidhi
gari moja kwa kuwa anayo mawili na kama anataka Discovery (Land Lover)
wamuachie lakini wapate moja kwa ajili ya binti yao kuendea chuo,”
kilisema chanzo.
Akizungumza kwa jazba, mama mzazi wa Asia alisema, walimzawadia gari
hilo kwa kuwa wote walikuwa wanapenda tasnia ya filamu hivyo gari hilo
lingemsaidia yeye na mume wake katika shughuli zao.
“Kinachouma ni kwamba tusingefikishana hapa lakini tulishamuomba sana
Slim kurudisha gari hilo au ampe mwanetu gari lingine abaki na hilo kama
analipenda lakini alikataa na mbaya zaidi ana kila kitu, kuanzia
ufunguo na kadi ya gari kitu ambacho hatendi haki kwa mtoto wetu,”
alisema mzazi huyo.
kizidi kutema cheche mbele ya kinasa sauti cha Ijumaa, mzazi huyo
alisema licha ya Slim kwenda Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata)
kushtaki ili arudiane na binti yao, haitawezekana.
“Nashindwa kuelewa kabisa jambo hili nilijitahidi sana kulivumilia
lakini nimeona imeshindikana kabisa hivyo tuliamua kwenda nyumbani na
kumchukua kumfikisha kituoni hapa maana sisi tulimfanya kama mtoto wetu
lakini yeye amekuwa mkaidi,” alisema mama huyo.
Mwandishi wetu alimfuata Slim kituoni hapo na kuzungumza naye kuhusiana
na sakata hilo ambapo alisema anachofahamu yeye ni kwamba zawadi
inapotolewa kwenye harusi na wazazi inakuwa ni ya mke na mume lakini
anawashangaa wazazi hao kuidai ikiwa hata mkewe hajampa talaka.
“Nashindwa kuelewa kabisa kwa sababu wazazi wa mke wangu walitoa gari
lile kama zawadi sasa sielewi kwa nini walidai tena wakati mke wangu
sijamuacha, suala hili lipo Bakwata.
“Isitoshe, gari hilo nimelitengeneza sana mpaka kufikia lilivyo sasa
kwani bado lipo gereji, lakini kwa kuwa wameamua kunidai, baada ya miezi
mitatu nitakuwa nimewapa gari lao,” alisema Slim.
No comments:
Post a Comment