Na Deogratius Mongela
KW/RB/8441/2014 imemshikilia
Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashimu Lundenga kwa madai ya
kuzichapa na Miss Tanga 1997, Mona Faraja ambaye pia ni mke wake na
kumsababishia majeraha, Risasi Jumamosi lina ‘full’ stori.
Miss Tanga 1997, Mona Faraja anayedaiwa kujeruhiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashimu Lundenga.
Ishu hiyo
iliyonyakwa laivu na majirani ilijiri usiku wa Jumatano iliyopita
maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar, nyumbani kwa Lundenga wakati wawili
hao walipokuwa wamepumzika baada ya mihangaiko ya mchana kutwa.Kwa
mujibu wa mtoa habari wetu, wakiwa wanabadilishana mawazo, mara simu ya
Lundenga iliita na ndiyo chanzo cha mtafaruku, upi huo?
TUJINGE NA CHANZO
Mtoa
habari wetu alisema kuwa, tatizo lilikolea mara baada ya simu hiyo
kuita mfululizo kwa namba ngeni iliyodaiwa kuwa ni ya ‘kichenchede’ cha
pembeni huku bosi huyo akiwa hana mpango wa kuipokea.SOMAZAIDI>>
“Mke wa
Lundenga alikuwa na shauku ya kujua nani anayepiga simu ya mumewe muda
huo na kwa nini mumewe haipokei lakini wakati akiendelea kujiuliza ndipo
ikaingia meseji ambapo inadaiwa Lundenga alikwenda ‘fasta’ kwenye inbox
na kuifutilia kwa mbali.
“Kitendo
cha kufuta SMS hiyo nacho kilitibua kabisa hali ya hewa, Mona akataka
kujua kwa nini mumewe alikuwa hataki kupokea simu na SMS iliyoingia
ilitoka wapi?
“Mona
akawa mkali baada ya kuona haridhishwi na majibu ya mumewe ndipo
alipoanza kutoa maneno yenye shutuma kwa mzee mzima ambapo naye
uvumilivu ulimshinda kama binadamu wengine, wakaanza kutwangana,”
kilisema chanzo hicho.
MKE AWAHI POLISI
Chanzo
hakikuwa tayari kuweka ‘fullstop’, kiliendelea kumwaga mchele kwenye
kuku wengi kuwa, baada ya mke kuona anazidiwa kwa kushushiwa makonde
mazito yaliyomvimbisha uso, usiku huohuo alikimbilia Kituo cha Polisi
Kawe, Dar kumripoti mumewe.
POLISI WAMKAMATA LUNDENGA
Mara
baada ya mke kumaliza malalamiko yake kituoni hapo, saa chache baadaye
polisi walifika nyumbani wakiwa na difenda ambapo walimchukua
mlalamikiwa huyo hadi kituoni kujibu madai hayo.
“Polisi
hawakuwa na maneno mengi, walipofika nyumbani walimkamata Lundenga na
kwenda kumlaza kituoni kwa ajili ya hatua nyingine za kisheria,”
kilisema chanzo.
MAJIRANI WANENA
Baadhi
ya majirani waliolitambua sakata hilo walionesha kushangazwa huku
wakimhurumia Mona ambaye alikuwa ameumia usoni, hususan mzunguko wote wa
jicho la kushoto.
MKE AINGIWA NA HURUMA
Wakati
gazeti hili likiwa katika hatua za mwisho kuelekea mitamboni, Mona
alidaiwa kuingiwa na huruma kwa kitendo cha kumlaza mumewe kituoni hivyo
alikwenda kwa lengo la kumfutia mashitaka.
“Mke
alimuonea huruma mumewe licha ya kupewa kipondo maana wamedumu kwenye
ndoa kwa zaidi ya miaka 10 sasa, si mchezo. Alikwenda Kawe kufuta kesi
lakini polisi wakamkomalia kwamba ishu lazima ifike mahakamani,”
kilisema chanzo.
Mwandishi
wetu alifika kituoni hapo na kukuta polisi na Mona wakiendelea na
mazungumzo lakini hadi tunakwenda mitamboni, Lundenga alikuwa bado
anashikiliwa kituoni hapo.
MKE WA LUNDENGA
Juzi, Risasi Jumamosi lilimpigia
simu Mona kwa lengo la kutaka kumsikia anasemaje kuhusu madai hayo,
lakini baada ya maelezo marefu ya mwandishi, alikata simu na baadaye
kuizima kabisa!Chanzo GPL
No comments:
Post a Comment