
Kiungo
wa zamani wa Yanga, Athumani Iddi Chuji na mshambuliaji wa zamani wa
Simba, Betram Mwombeki wamefeli majaribio ya kucheza soka la kulipwa
nchini Oman na imeelezwa sababu tatu ni chanzo.
Tayari
Chuji na Mwombeki wametua jijini Dar wakiwa kwenye pipa la Oman Air
ambalo limetokea katika jiji la Muscat kupitia Zanzibar.
Wawili hao pamoja na kiungo wa zamani wa Simba, Jerry Santo wote wamefeli kuichezea timu ya Oman Club iliyo daraja la kwanza.
Taarifa zinaeleza, Chuji ndiye pekee alionyesha kiwango kizuri na ilibaki kidogo tu aingie mkataba na klabu hiyo kongwe ya Oman.

Lakini
katika mechi ya mwisho akashindwa kuonyesha kiwango, hali iliyowafanya
wahusika kuahirisha na kumuungaisha katika kundi la Santo na Mwombeki.
Sababu tatu:
Moja:
-->
Inaelezwa Santo na Mwombeki walionekana wazi hawakuwa na stamina wala mazoezi ya kutosha.
Kwani walikuwa wanachoka mapema mazoezini hali iliyoanza kumpa hofu kocha ingawa wao walilakamika kuhusiana na hali ya hewa.
Mbili:
Mwombeki
alionekana mzito sana wakati Santo alishindwa kukaba labda kutokana na
kutokuwa fiti. Chuji anaelezwa kujitahidi katika mazoezi, huenda kwa
kuwa alifanya mazoezi ya kutosha akiwa jijini Dar es Salaam.
Tatu:
Walicheza mechi mbili za kirafiki, lakini wakashindwa kabisa kuonyesha uwezo.
Chuji pekee ndiye alicheza mechi ya kwanza vizuri na kuwapa matumaini viongozi wa Oman Club.
Santo na Mwombeki walishindwa kuanzia mechi ya kwanza, ile ya pili ambazo zote timu yao ilitoka sare wakaharibu kabisa.
Chuji naye alifanya vizuri mechi ya kwanza, lakini ile ya pili, kiwango kikawa chini.
TAARIFA:
Chuji
na Santo walitaka kuendelea kubaki Oman ili watafute timu nyingine,
wakati Mwombeki alisisitiza kwamba anataka kurejea nyumbani tu.
Hata hivyo ikashindikana, hivyo wote wakalazimika kurejea mwakwao Tanzania na Kenya.
Mwombeki
na Chuji wakaingia kwenye Oman Air iliyopitia Zanzibar, wakati Santo
akajitupia kwa Emirates ambayo imepitia Dubai hadi Nairobi.
Hata hivyo hadi Chuji na Mwombeki wanaondoka katika jiji la Muscat, Santo aliendelea kuwepo jijini Muscat na haikujulikana kama kweli aliondoka au atapiga kona abaki na kuendelea kusaka timu.
No comments:
Post a Comment