Mtangazaji mahiri Bongo, Gardner Gabriel Habash ‘G. Habash’ akiwa na Miss Mara 2000, Rashida Wanjara.
Gardner
Gabriel Habash ‘G. Habash’ na ‘mtalaka’ wake, Judith Wambura Mbibo
‘Jide’, Jumamosi iliyopita walifanya tukio lililowashangaza watu
kufuatia kila mmoja kuingia ukumbini akiwa na kampani yake na kukwepana kama paka na panya, Amani liliwanasa kwa vile lilikuwepo.Tukio
hilo lililoamsha minong’ono kwa watu waliosoma mchezo mzima, liliibukia
ndani ya Ukumbi wa Ten Lounge (zamani Business Park) uliopo Makumbusho,
Kijitonyama jijini Dar es Salaam ambako kulikuwa na uzinduzi wa albamu
ya Bongo Fleva.
Katika
hali isiyokuwa ya kawaida, Gardner alipoingia alikwenda kukaa kwenye
meza na watu wengine watatu, baadaye akafika Miss Mara 2000, Rashida
Wanjara na kuunga ambapo walikuwa wakibadilishana mawazo na kufunguliana
vinywaji kwa meno na kumiminiana kwenye glasi.
JIDE NAYE
Wakati Gardner ambaye pia
hujulikana kwa jina la utani la Kapteni akiendelea kujipoza na Rashida
na wengine, Jide yeye alikaa meza moja na kijana mmoja aliyevalia shati
la kitenge la mtindo uliowahi kutamba miaka mitano nyuma, wengine huita
Mackezie sanjari na wadada wawili.
No comments:
Post a Comment