Jamaa mmoja anayetumia majina ya Baraka, Muba au Martha Peter
amenaswa kwa kujipatia pesa kiudanganyifu akijifanya Ofisa wa Bodi ya
Mikopo wa Chuo cha Ardhi kilichopo jijini Dar.Tapeli anayetumia majina
ya Baraka, Muba au Martha Peter. Tukio hilo lilitokea Septemba 19 mwaka
huu katika Kituo cha Afya cha Kimara baada ya tapeli huyo kumlaghai dada
mmoja aitwaye Wema Raymond wakutane hapo kwa ajili ya vipimo vya ukimwi
vilivyotakiwa kuambatanishwa katika fomu ya kuomba nafasi ya kazi
ambayo awali dada huyo alidai kupatiwa na tapeli huyo.
Akizungumza na waandishi wetu, Wema alisema alimfahamu tapeli huyo
kupitia kwa rafiki yake aliyemtaja kwa jina la Rebecca, ambaye naye
awali alipigiwa simu na mtu huyohuyo akimtaka kimapenzi.
Wema alisema kuwa rafiki yake alimkatalia tapeli huyo, lakini siku
chache baadaye alimpigia tena akimwambia kulikuwa na nafasi ya kazi
katika Chuo cha Ardhi hivyo anamhitaji yeye kwa ajili ya nafasi hiyo.
“Kwa sababu Rebecca ana kazi yake tayari aliamua kunitaarifu mimi kwa
kuwa anajua natafuta kazi,” alisema Wema.Alisema alikutana na jamaa
huyo ndani ya Chuo cha Ardhi na kupatiwa fomu aliyoelekezwa kujaza kisha
akatakiwa kutoa shilingi 280,000 kama malipo ya fomu hiyo na gharama za
mafunzo ya siku tatu ya vitendo kuhusu kazi, fedha ambazo hakuwa nazo
kwa muda huo na kulazimika kumuomba rafiki yake Rebecca amsaidie.
Wema Raymond aliyetapeliwa na tapeli huyo anayefahamika kwa jina la
Baraka au 'Muba'. “Baada ya kumaliza mazungumzo pale chuoni
akanisindikiza hadi nje

No comments:
Post a Comment