27 September 2014

Cristiano Ronaldo na Gareth Bale kuingia Tanzania mapema mwakani Cristiano Ronaldo na Gareth Bale kuingia Tanzania mapema mwakani


Mashabiki wa mpira wa miguu nchini walikuwa na sababu kubwa ya kufurahi mwaka huu pale wachezaji wa zamani wa Club ya Real Madrid kuingia nchini na kuchuana na waliowahi kuwa wachezaji wa timu ya Taifa, ‘Taifa Stars’.
Kabla mwaka haujaisha, mmiliki wa Tanzania Sisi Nyumbani (TSN), Farouk Bonghoza ambao waliwezesha ujio wa wachezaji hao, amewaahidi mashabiki wa soka nchini kuwa January 2015 au July 2015 watawaleta washambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo na Gareth Bale.

Boghoza ameweka wazi mpango huo leo katika kipindi cha Sun Rise cha 100.5 Times FM alipofanya mahojiano na Fadhili Haule, Samira Suleiman na MC PiliPili.
“Tuombe Mungu, kuna jambo jingine inshallah kubwa litatokea. Halipo wazi lakini tuombe Mungu, kama sio January basi itakuwa July… wao wenyewe Real Madrid, Cristian Ronaldo na Gareth Bale.” Amesema Farouk Bonghoza.
SunRise ya 100.5 Times FM inakuwa hewani Jumatatu hadi Ijumaa, saa 12 asubuhi hadi saa 3 kamili asubuhi.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname