Mwanasheria mkuu wa CHADEMA akizungumza na wanahabari muda huu |
Chama cha democrasia
na maendeleo CHADEMA leo kimetangaza kuwa mwenyekiti wao keshoi ataenda
polisi makao makuu kuitikia wito wa jeshi hilo ambao ulikuja kwa barua
ukimhitaji mwenyekiti huyo kufika makao makuu ya jeshi hilo.
Kauli hiyo
imetangazwa muda huu makao makuu ya chama hicho na wanasheria mkuu wa
chama hicho mbunge TUNDU LISSU wakati akizungumzia wito wa jeshi la
polisi kumhitaji mwenyekiti wao kwa kile ambacho ameadi kuwa hakijawekwa
wazi wanamwitia nini.
"Tumepokea barua ya
jeshi la polisi makao makuu wakimtaka mwenyekiti wetu kufika makao makuu
ya polisi kwa maelezo,kamati kuu ya chama imeridhia mwenyekiti aende
ila hawezi kwenda mwenyewe hivyo wanasheria wote wa chama walioko mkoani
Dar es salaam watamsindikiza kwa ajili ya kujua mwenyekiti wetu
ameitiwa nini.hivyo tunaomba wanasheria wote wa chama kesho tukutane
polisi makao makuu saa tano kwa ajili ya kumsindikiza.
Naibu katibu mkuu wa chama JOHN MNYIKA akizungumza |
Aidha naibu katibu
mkuu wa chama hicho mh JOHN MNYIKA NAYE naye amewataka wananchi na
wapenzi wa chama hicho kujitokeza kesho kumsindikiza mwenyekiti wao kwa
ajili ya kusikiliza kile ambacho mwenyekiti wao ameitiwa nini na jeshi
la polisi
NA Habaari 24
No comments:
Post a Comment