Mwanadada anayefanya poa katika tasnia ya filamu za Kibongo Salma Jabu ‘Nisha’.
MWANADADA anayefanya
poa katika tasnia ya filamu za Kibongo Salma Jabu ‘Nisha’ hivi karibuni
alilazimika kuwachezea wanafunzi waliomtaka kufanya hivyo wakati wao
wakimuimbia katika maeneo ya Posta, jijini Dar es Salaam.Akizungumza
na gazeti hili, Nisha alisema aliteremka kwenye gari kwa ajili ya
kuuliza sehemu aliyokuwa anataka kwenda, ghafla wakajitokeza vijana hao
ambao ni mashabiki wake waliomtaka akate kiu yao.
“Ile
kushuka ili niulizie sehemu nikashangaa kundi la wanafunzi limenivamia
na kuanza kuniambia Nisha shuka huku wakiimba na kunitaka niwachezee,
ikanibidi nifanye wanavyotaka baada ya hapo wakanielekeza nikaondoka,
kiukweli nilifurahi na napenda sana kuona mashabiki zangu wakinipa
sapoti,” alisema.
No comments:
Post a Comment