Mashindano ya Serengeti Fiesta Super Nyota Divaz ni miongoni mwa
vihusishi vya tamasha la Serengeti Fiesta ambalo kwa Shinyanga bado
halijafanyika kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya matatizo
yaliyotokea Musoma ya ajali ya mabus mawili.
Upande wa Shinyanga washiriki waliojitokeza jumla yao ni 10 ingawa
kuna wengine walichelewa kuchukua fomu kutokana na kutofahamu siku rasmi
ya mashindano,round ya kwanza ilikamilika kwa washiriki 4 kutolewa.
Mpaka round ya mwisho ambayo ilikua ya 3 majaji wakiongozwa na Dj
Fetty walimtangaza Amina kama mshindi wa Serengeti Fiesta Super Nyota
2014 kwa mkoa wa Shinyanga.
Mashindano haya yalifanyika Club Butiama ya hapa Shinyanga,Hizi ni baadhi ya picha wakati mashindano yakiendelea.
No comments:
Post a Comment