02 August 2014

Video: Mchezaji wa mpira wa kikapu Paul George avunjika vibaya mguu, vilio vyatawala

Mchezaji wa timu ya mpira wa Kikapu ya Indiana Pacers t ya Marekani, Paul George amevunjika vibaya mguu wa kulia Jana usiku katika mechi za mpira wa kikapu za Marekani huko Las Vegas.
Mchezaji huyo aliumia vibaya wakati akimkimbiza James Harden na kuruka kwa haraka akiwa katika mwendo mkali ili kumzuia asifunge, ndipo alipopitiliza na kujigonga vibaya.

Tukio hilo lilizua hisia kali za majonzi kwa mashabiki wachezaji wa timu zote ambao wengine walishindwa kuvumilia na kutokwa na machozi kwa jinsi mguu huo ulivyooneshwa ukiwa umepinda vibaya.
Baba na mama yake Paul George pia walihudhuria mechi hiyo na walionekana waliumia zaidi baada ya kuona mtoto wao akibebwa kwenye huku video iliyokuwa ikionesha kwa ukaribu tukio hilo ikiwa mwiba zaidi katika hisia zao
Kwa mujibu wa SportsCenter, mchezaji huyo alifanyiwa upasuaji na kuwekewa pini maalum ili kuurekebisha mguu wake mfupa ulivunjika kama muwa uliopindishwa kwa nguvu.
Hata hivyo, asubuhi ya leo, Paul George amewafariji mashabiki wake baada ya kutweet akiwaeleza kuwa atapona na kuwa mzima zaidi ya zamani huku akiwashukuru kwa sapoti yao.
“Thanks everybody for the love and support.. I'll be ok and be back better than ever!!! Love y'all!! #YoungTrece.” Ametweet Paul Geoge.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname