02 August 2014

ANCELOTTI: LAMPARD ATAKUWA USAJILI MKUBWA KWA MANCHESTER CITY

Ancelotti: Lampard would be a top signing for Man City
CHANZO MPEJA BLOG
BOSI wa Real Madrid, Carlo Ancelotti anaamini Manchester City itakuwa imelamba dume kama itamsajili kiungo mkongwe Frank Lampard ambaye yuko mbioni kujiunga Etihad kwa mkopo.
Kiungo huyo mwenye miaka 36 aliachwa na Chelsea majira haya ya kiangazi mwaka huu baada ya mkataba wake kumalizika na alisaini mkataba wa miaka miwili na New York City FC mwezi juni mwaka huu.
Manchester City na New York Yankees wote wana hisa za umiliki wa New York.Msimu wa ligi wa Marekani unatarajiwa kuanza mwezi machi 2015, hivyo Lampard anatakiwa kujiunga na kikosi cha Manuel Pellegrini kwa mkataba mfupi wa mkopo ili kulinda kiwango chake.
Ancelotti aliyemshuhudia Lampard akiwa mfungaji wa juu zaidi wakati yupo Stamford Bridge, anaamini nyota huyo wa kimataifa wa Uingereza atakuwa msaada kwa Man City na akatania kuwa anaweza kumsajili Real Madrid.
“Sikujua hili. Nimeshangaa sana kwasababu nilijua anakuja kucheza Marekani,” Alisema Ancelotti ambaye yupo Michigan kukabiliana na Manchester United.
“Nimechelewe sana, ningemsajili Real Madrid, lakini nimfurahia sana Frank kwasababu nina kumbukumbu nzuri juu yake. Namtakia kila la kheri. Ni usajili mzuri kwa Manchester City”.

Lampard alicheza miaka miwili chini ya Ancelotti na kuiona Chelsea ikishinda kombe la ligi kuu, kombe la FA na Ngao ya Hisani kabla ya kutimuliwa baada ya kumaliza msimu wa 2011 bila kikombe.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname