14 August 2014

UKATILI: KIGOGO AMCHOMA KISU MKEWE, KISA KINASHANGAZA SANA! SOMA ZAIDI HAPA!

Mke wa kigogo (Mugaka),Bi. Leah aliyefanyiwa unyama na mumewe.
KIGOGO wa shirika moja la kimataifa linalojishughulisha na watoto yatima, tawi la mkoani Pwani, Tanzania aliyetajwa kwa jina moja la Mugaka, anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 35 hadi 40, ametupwa rumande akituhumiwa kumchoma kisu na kumtoa manundu mkewe, Leah (28).Tukio hilo la kusikitisha lilijiri wilayani Kisarawe, Pwani mwishoni mwa wiki iliyopita. Kwa mujibu wa habari zilizopatikana, chanzo cha unyama huo kinashangaza huku madai ya Mugaka ambaye ni afisa mshauri wa shirika hilo yakisema mkewe huyo amekuwa akimjazia choo kwa kuwa tangu amuoe miaka mitatu iliyopita, ameshindwa kumzalia mtoto.

Sehemu ya mguu alipochomwa kisu na Bw. Mugaka (mumewe).
 Habari ziliendelea kudai kwamba shirika analofanyia kazi Mugaka linalosimamiwa na mfuko wa rais wa zamani wa Marekani, Bill Clinton. Madai mazito yalishushwa kwamba Mugaka amekuwa akimnyanyasa mkewe kwa sababu hiyo, kiasi cha kumtolea maneno ya kejeli, dharau, kashfa huku akimshushia kipigo ‘hevi’.SOMA ZAIDI>>

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname