14 August 2014

MGONJWA WA EBOLA' ASABABISHA TAFRANI SHINYANGA

Wakazi wa Manispaa ya Shinyanga, kwa siku mbili mfululizo walikumbwa na kiwewe, baada ya kuenea uvumi kwamba kuna mgonjwa wa mwenye homa hatari ya ebola, aliyefikishwa katika Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga. 
Taarifa za kuwepo kwa mgonjwa huyo, zilidai kuwa mgonjwa huyo alitoka katika moja ya mitaa ya Manispaa ya Shinyanga na  alikuwa akitokwa damu puani na mdomoni kabla ya kuzimia.
Akizungumzia hali hiyo jana, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dk Ntuli Kapologwe alisema mgonjwa huyo ambaye alikuwa akitokwa damu mdomoni na puani, alifika hospitalini hapo juzi na baada ya kufika wauguzi na madaktari walitaharuki.
Kwa mujibu wa Dk Kapologwe, mgonjwa huyo alipelekwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU), huku baadhi ya wauguzi na madaktari wakimkimbia hali iliyotia hofu kwa baadhi ya wahudumu na hata wagonjwa hospitalini hapo.
Hata hivyo, Dk Kapologwe alisema baada ya uchunguzi wa awali, ilibainika kuwa mgonjwa huyo ana matatizo ya kutokwa damu mara kwa mara na hajaambukizwa virusi hao wa ebola.SOMA ZAIDI>>

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname