13 August 2014

NYANI WA AJABU AJITOKEZA JIJINI DAR, AFANYA KAZI YA UBEBAJI TAKA MTAANI, CHEKI PICHA ZA TUKIO HAPA



KATIKA pitapita za waandishi wa Website ya masainyotambofu.com jana majira ya saa tisa alasiri walikumbana na nyani waa ajabu katika moja ya mitaa ya Tabata jijini Dar, Nyani huyo alieonekana kuwa mchangamfu kama amemwagiwa ndimu alifanya mambo ya kustaajabisha uma kwani wengi walimshangaa nyani
anaeletewa vifurushi vya takataka na wakazi wa mtaani hapo na kuvipakia mwenyewe kwenye mkokoteni kama binadamu huku akiwa na kibox kilichoandikwa (WEKA PESA HAPA TSH.200/=) Hio ikiwa ni malipo ya uzoaji taka.

Huo hapo ndio muonekano wa Box alilofungiwa kwenye mkokoteni kwa ili watu wawe wakitumbukiza pesa humo, Ama kweli dunia ina mambo yani mtu amekaa akafikiri, Akaamua kubuni mbinu mbadala ya kujitafutia kipato kwa kumfuga nyani na kumpa mafunzo ya aina hio, Sasa swali linakuja kwako ewe ndugu msomaji kuwa unahisi Nyani huyu analipwa mshahara kwa kazi hii anayofanya au anaambulia msosi tu?..

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname